Mwezi wa Kwanza 1

Swahili

                                                                                                          Mwezi wa Kwanza    1
KUTAFAKARI KWA KINA
Masomo: Zaburi sura 1 na sura 2; Mathayo sura I


     Hii ni asubuhi ya mwanzo, ni mwanzo wa mwaka mpya, ni mwanzo wa utaratibu wetu wa kusoma Biblia kila siku; kwa kawaida ni muda ambao  ni wa kutafakari kwa kina. Kwa kawaida huwa tunatazama nyuma na  kuangalia mbele, tunapoangalia nyuma miezi kumi na mbili  iliyopita, kila mwanaume na mwanamke anaweza kujiuliza  yeye mwenyewe iwapo miezi hiyo kumi na mbili  ilikuwa ni miezi kumi mbili ya mafanikio  kiroho au  ilikuwa miezi kumi na mbili ya kudumaa au ilikuwa miezi kumi na mbili ya kukua katika kweli— ni na maana ya mafanikio ya kiroho maana hakuna mafanikio mengine ya kukua, hata kama  yanaweza kuwa ya muhimu kwa upande wa kimwili, kwa kweli haitaweza  sasa kulinganishwa katika mizani ya kukua katika kweli katika sifa zile ziletazo amani na haki , na furaha isiyoneneka na yenye maisha bora ya wakati ujao unaongojewa wa milele, kwamba tunauona au la.

     Ni swali ambalo kila mtu peke yake anaweza kujiuliza; yeye mwenyewe anajua alivyo katika maisha ya kiroho, na jinsi anavyoendelea: hajidanganyi mwenyewe kwa muonekano wa nje ambao unaweza kuwapotosha wanaomtazama.

      Jinsi gani tunavyoendelea kiroho ni suala la kipimo tunachotumia, hii hudhihirisha kukua kiroho na mwenendo wetu ulivyo. Mtu mwenye vipimo vya busara atakuwa ni mtu mwenye mafanikio katika busara. Ni vipimo gani vya busara katika jambo hili la kiroho? Je inatupasa tuelekeze vipi hatua zetu ili kuhakikisha kwamba mwisho wa miezi kumi na mbili tuwe tumekaribia zaidi ya hali ya kiroho na kuacha nyuma zaidi na zaidi hali ya tabia ya mtu wa mwilini? Tuna jibu hasi (hapana) katika Zaburi tuliyokwishaisoma, na kuna jibu chanya (ndiyo) pia; hatutapoteza muda katika  kuangalia majibu haya.

     Jibu la kwanza linatuambia ni mambo gani tusiyatende, ili tuifikie hali ya baraka ya kweli. “Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki;Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha”. Hapa kuna kwenda, kusimama, na kuketi, maneno haya yametumika kuelezea hali halisi ya mwenendo wa maisha yote kiroho. Wazo hili ni uthibitisho rahisi kiasi kwamba hata mtu mwenye akili ndogo kabisa anaweza kulielewa. Kila mmoja anaelewa ni akina nani wasio mcha Munga—wenye mizaha, wenye dhambi; na kila mmoja anajua nini maana ya kutoshiriki tabia zao ; na wala hakuketi katika baraza lao, na wala hakusimama katika njia zao.
Tatizo kamwe siyo katika kufahamu inamaanisha nini, bali ni kutenda lile jambo linalomaanishwa. Kwa kutenda ile maana hakika ni mwenendo wa maisha ya kiroho ambao ni mgumu na pia ni mwenendo unaolaumiwa na wengi wasio mcha Mungu. Mwenendo huu mzuri unalaumiwa na  unaonekana kuwa ni mgumu kwa wenye akili finyu; lakini ule mwenendo usiofaa huonekana kuwa ni  wenye  uweledi na unaojali haki na uhuru wa watu; kwa hiyo sasa tujiulize ni nani tunayepaswa kutii— Maandiko Matakatifu(Biblia)  au ulimwengu— tumtii Mungu au mwanadamu.

      Yesu alisema waziwazi kuhusu umuhimu wa kutenganisha maisha ya kiroho na maisha ya dhambi.  Sisi sote tunafahamu maneno ambayo kamwe hayawezi kurudiwa-rudiwa mara kwa mara wakati huu tulionao wa hali dhaifu ya matazamio: kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. “Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.”.Je,sisi tumechaguliwa kutoka ulimwenguni? Ikiwa hatukuchaguliwa tusiwe wa ulimwengu, basi,hatuna tumaini. Na kama tumechaguliwa, inatupasa tukubali kuchukiwa na tusishindwe na jaribu la kujipenda wenyewe au tusiwe na ubaguzi wa rangi au kabila ili tuweze kusemwa vizuri.

      Tunafahamu pia maneno mengine ya Mungu, yaliyosemwa na mtume Paulo, “Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike.”
Tumeusikia mwaliko huu, na tumeukubali. Iwapo tumeupokea, sisi “tumetengwa kwa ajili ya BWANA” na ni lazima kwa ujasiri  tukubali  nafasi hii ya neema bila kujali wanasemaje wasitaarabu na wasiokuwa wasitaarabu, wataalamu wa sayansi na wasiokuwa  na elimu ya sayansi, watu wenye elimu na hofu itokanayo na  hisia potofu za nchi   katika kizazi  hiki tunamoishi.
       
      Hali halisi ya kundi hili teule inatamkwa waziwazi katika Maandiko jinsi walivyo; ni hali ya mwonekano wao ukiwaona; lakini unaweza kuwapata watu wachache. “Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku”. Neno “sheria” lina maana tofauti kwa wakati tofauti lakini kwa kawaida kila mahali lina maana moja linapotumika; yaani, neno la Mungu linapotamkwa kwa ajili ya kumuongoza mtu. Mungu alitamka neno moja ili kuwaongoza  Israeli, na ametamka lingine kwa ajili ya kutuongoza sisi. Maneno yote mawili ni sheria ya BWANA, na ingawaje sheria ya Musa haitufungi sisi, hata sheria hiyo ya Musa inaeleza kwa kiwango cha juu  sana cha furaha ya mwanadamu. Ni somo lenye faida watumwa Mungu kulitafakari mpaka siku zetu hizi. Tukichukua msemo wa sasa, msitari huu ungesomeka hivi: “Bali Biblia ndiyo impendezayo, Na Biblia huitafakari mchana na usiku”. Jinsi kundi kubwa la Wakristo linavyoliainishwa vibaya neno hili, hasa hapa Birmingham, tunafahamu. Pia tunafahamu kuhusu jambo fulani kuhusu matokeo ya hekima hii ya kupenda Neno la Mungu.  Kuna maelfu ya watu duniani wanaosoma Biblia pamoja nasi kwa kutumia “Mwongozo wa kusoma Biblia” na wengi sana wamethibitisha kuwa wanasoma kwa furaha.
    
    Je, ni kila muumini aliyehudhuria hapa aliyejipatia heshima na haki ya kufuata kwa dhati  utaratibu huu wa maisha wa kusoma Biblia kila siku katika muda wa miezi kumi na mbili iliyopita? Inawezekana jibu la wengi ni la kweli na la kutoka moyoni kabisa “Ndiyo”, lakini kwa wengine tunaweza kuwa tulishindwa na kuazimia ya kwamba miezi kumi na mbili ijayo itakuwa miezi ya kusoma Biblia kila siku. Kwa njia hii pekee, inawezekana, katika kizazi kama chetu, tukajiokoa kutokana na uovu uliopo ulimwenguni. Hatuwezi kuyafuata mawazo ya Mungu wakati huu isipokuwa kwa kusoma na kuamini Biblia; mambo mengine yote ni akili ya mwanadamu, iliyodanganywa na maneno matupu ya uongo na ahadi za uongo. Hakuna faida yoyote kwa mtenda dhambi bali huleta matokeo ya uchungu na kifo kutokana na kuenenda katika njia za giza, haijarishi njia hizo zinang’ara kiasi gani na zinapendeza kiasi gani. Ni mawazo ya Mungu peke yake, yanayokubaliwa, kwa dhati na hutekelezwa kwa kusoma na kutafakari kila siku  mawazo ya Mungu, yawezayo kuleta amani na furaha hata katika maisha haya, na kwa ajili ya maisha yanayokuja, na hapa ubishi unashindwa kabisa kutokana na nguvu ya Mungu ipitayo nguzo zote.
      
   Ikiwa kumcha Mungu hakuna faida, tunayo kila sababu ya kumcha Mungu. Na kamwe Mungu hamwambii mtu yeyote, afanye jambo lolote bila kutumia nia ya kutosha itokayo kwenye uongozi na upendo wa Mungu Mwenyezi, mwenye hekima, na Mungu mwenye upendo kwa watu wote. Zaburi nayo, inarejelea tabia ya mtu asikwenda katika  mashauri ya wasio haki. “Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa”.
Hii ni lugha ya mfano; lakini maana yake ni wazi mno inaweza kutoeleweka. Tunao uzoefu mdogo katika nchi yetu yenye unyevunyevu kuhusu tofauti kati ya mti uliopandwa kando ya mto na mti uliopandwa mbali na maji. Upande wa mashariki, wasafiri wanasema, tofauti inaonekana sana; mti uliopandwa karibu na mto una hali ya kusitawi na kuzaa matunda;  na ambapo ule mti uliopandwa mbali na maji una mwelekeo wa kutokusitawi vizuri na hudumaa. Ni kwa maana ipi mtu ampendaye Mungu anakuwa kama mti uliopandwa karibu ya mto? Hili lina muonekano uliopo, usio tia shaka, katika amani idumuyo na upya wa maisha ambayo huonekana pekee kwao wanaomtanguliza Mungu maishani mwao.Lakini utekelezji wake ni lazima hatimaye uwe ni katika siku zijazo; ndivyo ilivyowekwa katika Zaburi kwa ulinganisho unaowatofautisha wamchao Mungu na wasiomcha Mungu. Inasema, “Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.” Kwa hiyo ni siku ya kusanyiko la wenye haki, na ni siku ya kuwaangamiza watenda maovu katika hukumu inayokuja. Hili likiwa hivyo, hakuna ugumu kuutambua mto, pamoja na kufanikiwa. Ni mfano uliotumiwa katika Ufunuo. Mto unaotoka katika kiti cha Enzi cha Mungu katika mfano huo “mto safi wa maji ya uzima, unang’ara mithili ya bilauri”. Miti iliyopandwa ukingoni mwa mto huo ni wacha-Mungu, ambao wamo ndani ya uhusiano wa kweli na chanzo cha chemchemi ya uzima, ya kwamba wao wanaoishi na kubakia ndani ya uzima na kuwa na nguvu za Mungu mwenyewe, ambaye wamemkaribia sana kwa nguvu za milele. Kwa maana ya moja kwa moja inamaanisha ile hali ya kubadilika na kuwa na uzima wa milele kwa Roho wa Mungu, ambaye tumeahidiwa katika nyaraka za mitume.

Kwa muda mfupi, fikiria, ulinganisho wa kufurahisha (au kupendeza) wa kuwa katika hali hii  ya maisha tunayoishi sasa hivi maana imeandikwa, “Moyo hufahamu uchungu wake wenyewe”. Kwa kweli, tunaweza kusema kwamba kila mtu anauelewa udhaifu wa uhai wake wa kimwili (wa kifo), na udhaifu wake wa kiroho,sisi tunahisi kuwa maisha siyo makamilifu na kuwa maisha  ni jambo la muda mfupi, na ndivyo tunavyoona kila tunapoangalia mambo yanayotuzunguka.
Kuna baadhi ya watu sasa hawapo muda huu  ambao tulikuwa nao katika miezi 12 iliyopita; wako wapi sasa,  lakini msajili wa kumbukumbu makaburini ndiye anaweza kutuambia; wao wametoweka kutoka kwenye nchi ya walio hai; wametokomea kutoka kwenye nchi ya walio hai. Pia mwaka huu litakuwepo pia pengo kama hili hili mwaka ujao, isipokuwa kama Bwana atakuwa amekuja; ni akina nani ambao hawakuwepo(watakuwa wamefariki) hakuna anayeweza kueleza; inawezekana kuwa ni yeyote kati yetu, nasi mara tuondokapo kitabu chetu kidogo kinakuwa kimefungwa milele; hadi kitakapofunguliwa tena mbele yake Yeye ambaye ndiye Ufufuo na Uhai.
Kuna baadhi ya watu, neno hili la kutafakari kwa kina kwaoni jambo la kuhuzunisha. Kwa hekima haitakiwi kuwa hivyo, na wala isionekane hivyo. Kinyume chake, inaleta uchangamfu wa hakika na unaoweza kufunikwa juu ya maisha yetu haya ya ubatili. Maan huondoa huzuni ambayo imo ndani ya maisha yetu ya kifo; hutawanya giza linalogubika upeo wa kuona wa macho ya wanadamu wasio kuwa na Kristo; hutupatia nguvu ya kuushinda uovu wa sasa kwa  kusitahimili  na kushangilia kwa furaha  inayomaanisha siku zijazo za milele, na kutuletea hisia ya mvuto wa hali isiyowezekana kuwepo bila ya kumjua Mungu. Na ndivyo ilivyo kama Paulo alivyosema kwa ajili ya huduma ya kazi ya Kristo, ambayo ni“Kuwakomboa wale wote ambao kwa hofu ya mauti walikuwa chini ya Kongwa maishani mwao”.
Siyo tu huondoa hofu ya kifo, lakini huleta hamu ya kutamanisha kwa kiwango cha juu sana, kwa sababu mwanadamu yeyote hata kama atapata akipendacho  lakini  huongeza matazamio ya kuishi miaka elfu  inayo sababishwa na kifo  ingawa huwa bado yu hai kwa muda mfupi. Baadhi ya watu wanasema wanapenda kuishi mpaka Bwana atakaporudi. Hali ya kuhisia maisha ya kiroho  ingeonekana zaidi kama hisia yenyewe ingejikita katika kutamani ujilio wa Bwana tu. Ukichambua hisia hii, na wewe utaona ya kuwa chanzo chake ni hofu ya kifo. Pale ambapo imani na tumaini vina nguvu, hofu hii hushindwa, na kubadilishwa na kukubali kifo wakati wowote itakapompendeza Bwana kukiruhusu.
 Kukubali kwa furaha kwa ajili yake kuna maanisha kupokea imani na tumaini kuliko kuishi hadi Bwana atakaporudi. Inamaanisha kufutilia mbali matukio mawili ya mtu; yaani muda wake wa kuishi na kifo ambacho katika kifo hakuna tena uzima. Busara itumike, hukumu itakuwepo hapa moja tu.Ni kwa sababu akili ni dhaifu mno na ndiyo inayotawala watu wengi sana wakati wazo linapotolewa sura zao zinafadhaika na hazikubaliani. Kuishi mpaka Bwana atakaporudi ni kuingojea siku ya kurudi katika hali hii mbaya inayokatisha tamaa. Na kufa katika Bwana ni kuiendea siku ya Bwana pasipo kuingojea. Anayetarajia kupata kitu chema angependa akipate mapema bila ya kuchelewa.


 Anayetazamia kuitwa aingie ndani ya jumba la kifahari na kwa furaha akiwa ni kati ya wageni waliohudhuria angalipenda kuitwa mara moja kuliko kuachwa amesimama nje  akisubiri kwenye baridi na mvua mpaka wakati  jina lake litakapotajwa?
Hakuna mtu anayetambua ukweli wa kifo na kuwa na uhakika wa utukufu utakaofunuliwa Kristo atakaporudi, hawezi kusitasita hata kidogo kwa ajili ya wapagani wanaosema

Somo letu la Agano jipya linatuonyesha asili ya haya mapambazuko. Kama ilivyo kwa asili ndivyo ilivyo katika ukombozi wa mwanadamu. Mungu kwanza aliumba jua ili litawale mchana, na alifanya jua kwa uweza wa nguvu yake, yaani aliliumba kutokana na nguvu yake au kani, tunavyoweza kusema; jua siyo zao la mazingaombwe – hakuna kilicho hivyo; ni elimu ya dini inayofahamika sana kwamba Mungu aliumba vitu vyote kutokana na “kisichokuwepo” – aliviumba vyote vikatokea kwake yeye mwenyewe, na Mungu ni wa milele. Vitu vyote ni tumeambiwa muhtasari; kwa kutumia neno rahisi ya nguvu yake isiyoonekana, ya kuwa vitu vyote vilifanyika na kuongozwa kwa hekima yake. Jua la Kiroho tulijualo ni Bwana Yesu, na katika ufahamu wa juu zaidi, ambapo utangulizi jinsi alivyoumbwa ni wa namna moja kama alivyoumba vitu vingine.  Yaani na Yesu aliumbwa. Mungu amemuumba, na ametupatia Mungu mwenyewe ndani yake kama tunavyosoma “Ataitwa Immanueli, ambayo, ikitafsiriwa, ni Mungu pamoja nasi”. Ni uthibisho na uhakikisho  wa ukweli huu umewkwa bayana juu yetu, kwa kuwa muda baada ya muda, na kwa maneno ya Yesu na maelezo ya mitume wote. Wakati wote Yesu aliwasihi sana watu waliomsikiliza wakati uleule watatambue kuwa Baba yake alikuwa ndani yake na wala wasidhanie nguvu alizozionesha kuwa zilikuwa za kwake mwenyewe. Mitume kila wakati humwonesha kuwa Yesu alipewa jina lipitalo kila jina, ambalo kwalo kila goti litapigwa ili Mungu atukuzwe katika Kristo. Kwa hiyo, jua lililopampazuka juu ya usiku wa giza letu ni Mungu mwenyewe akiwa ndani ya Mwanaye wa pekee ambaye alizaliwa na Mariamu. Lakini utukufu kamili wa mapambazuko bado haujafunuliwa machoni mwetu. Dunia ya asili ilikuwa imefunikwa na giza na ukungu muda mrefu baada ya jua la asili kuumbwa; nalo jua, ingawa lilikuwepo hewani, halikuwa likionekana duniani. Giza lilitanda katika usawa wa “vilindi vya maji,” kwa hiyo ingawaje jua la haki limewekwa angani “giza linafunika nchi, na giza kuu(dhambi) linawafunika watu”. Hadi Kristo ajapo tena ndipo giza litakimbia. Ujio wake ndiyo itakuwa alfajiri angavu itakayomaliza usingizi wa watakatifu, usingizi wao mtamu na mfupi katika zama zote na katika kila nchi, ambao mara utakapokwisha, hautakuwepo usingizi tena milele. Ila asubuhi ile italeta siku ambayo haitaisha kamwe. Inaitwa siku yake Kristo, siku ya Bwana, siku ya wokovu. Daudi anasema, “Hii ndiyo siku Bwana aliyoifanya, siku ambayo anasema “wenye haki watakuwa na furaha”. “ Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana, Naam, mbele ya watu wake wote”.  Na hivi ndivyo furaha ya sura za wateule zitakavyokuwa – “Naam, mbele ya watu wake wote ”. Watu wote wa enzi zote watakuwepo hapo, wa kila ufalme na kila nchi, na wala hakuna atakayepungukiwa kitu. Lakini hataingia mtu yeyote aliye najishi, au mtenda machukizo ama mtu yeyote mwenye kutamani au asemaye uongo. Je,ndugu zangu, tutakuwako huko? Tunaweza kutumainia hilo; kwa kuwa tumealikwa; kuna masharti ya kuzingatia; siyo kuwa hatuyawezi, maana kila mmoja anatakiwa ajikane mwenyewe yaani aichukuie nafsi yake wakati huu. Siyo kwamba ni haiwezekani kupita katika njia ile, ingawaje ni nyembamba nao wanaopita katika njia ile ni wachache. Masharti yake yote ni ya kawaida na tena ni ya kuvutia sana, ni matamu mno. Mungu anataka tumwamini, tumpende, tumtukuze, na tuwe na imani katika ahadi zake, na tuwe wanyenyekevu na watiifu kwa kazi zake tunazopaswa kuzifanya,  na kutii amri zake na  tuimarike katika kufuata maagizo haya yote. Maana imeandikwa kuwa “wana amani nyingi waipendao sheria yako”. Je hatuwezi kuvutiwa na kila mtu ambaye amejibu kuwa ameyatekeleza haya? Hakuna jambo lolote isipokwa kuna amani na utamu unaotoka katika utu wa ndani wa mtu anayefuata njia ya kumcha Mungu. Mambo ya usumbufu waliyonayo wanadamu hisia bandia za kipindi kifupi na za majuto. “Kumcha Mungu ni faida katika maisha  haya,” wakati huu wa sasa na kwa wakati ule unaokuja.Ni nani asiyechagua kwenda katika njia ya baraka iliyotayarishwa kwa ajili yetu katika siku hii ya kufungua mwaka mpya, katika Zaburi ya kwanza ya Daudi, na mtu ambaye ameichagua njia hii, hatashindwa kutiwa moyo kusitahimili kwa kuvumilia ndani yake mpaka mwisho, na ambao wakisha ingia ndani yake na wakaiacha kwa ajili ya udhaifu wao na kwa ajili ya anasa za dunia, hawawezi wakajiponya  wakatoka katika njia inayoongoza kwenye mauti, na kurejea katika njia iongozayo kwenye mji mtakatifu? Hekima inawezakuwa na majibu haya na ni jibu moja tu kwa maswali haya, na kwa wale wanaojitahidi kuwa watoto wa hekima; ni jukumu letu kuongozwa na jibu la hekima— Robert Roberts.

 

Swahili Title
Mwezi wa Kwanza 1
English files
Literature type
English only
Month
D7 Node Id
1499