Fellowship - Lesson 01 - What is a Church?

Swahili

Ushirika–Kanisa ni nini?

Somo 1: Utangulizi – Kanisa ni nini?

Hii ni sehemu ya kwanza katika mfululizo wa masomo ishirini, yanayofanya kozi yanayofundisha kuhusu ushiriki wa jamuia ya Wakristadelfia. Mwanzoni kozi hii ilitayarishwa ili ipelekwe pamoja na kijarida cha Ekklesia kidogo kidogo. Kama unasoma haya ndani ya kijarida basi utegemea somo la 2 katika kijarida kitachofuata.

Katika somo hili tutajifunza haya:

 

Kama unasoma haya ndani ya kipeperushi basi tegemea somo la 2 katika kipeperushi kifuatacho ndani ya somo hili utaangalia haya:-

 • Ni kwa nini kozi hii imeandikwa

 • Kozi hii imeandikwa kwa ajili ya nani

 • Je,utafaidikaje kwa kusoma kozi hii

 • Sehemu kuu katika mafunzo haya inahusu nini?

 • Jinsi ya kutumia Kozi hii

 • Swali kubwa ni kuhusu “kanisa ni nini”?

Yaliyomo ndani ya kozi

Sehemu ya 1: Jumuia ya Wakristadelfiani ni nini?

 1. Utangulizi – kanisa ni nini?

 2. Ushirika

 3. Jumuia ya Wayahudi

 4. Msingi wa umoja

 5. Kutenda kama watumwa.

Sehemu ya 2: Kufanya kazi pamoja

 1. Ukarimu

 2. Kufanya maamuzi

 3. Kusuruhisha mgogoro

 4. Ukoloni

 5. Kubadilisha au kuhamia Ekklesia nyingine.

Sehemu ya 3: Meza ya Bwana

 1. Mkate na Divai

 2. Ushirika na Mungu

 3. Kushughulikia upweke

 4. Kuwafahamu waumini wako

 5. Ni nani mmiliki wa jengo?

Sehemu ya 4: Kazi zetu

 1. Kusanyiko la Ndugu

 2. Shule za Ekklesia

 3. Kuhubiri sehemu ya mbali

 4. Changizo

 5. Kuhubiri


 

Ni kwa nini kozi hii imeandikwa

Jumuia ya Wakritadelphia siyo kanisa kama yalivyo makanisa yanayotuzunguka. Ni jumuia ya kipekee katika muundo wake, na ni ya kipekee katika mpangilio wake. Ekklesia za Wakristadelphia hawana uongozi wa :Maaskofu,Mashemasi,Wachungaji,Wawakilishi, Mababa,Mapapa, Walimu, Marabi, Makuhani (maneno hayo kwa maana ya kanisa: Mathayo 23:7-8); na hakuna muumini yeyote aliye wa muhimu kuliko mwingine . Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu”. Wagalatia 3:28), naye Kristo ndiye aliye kichwa (Warumi 12,1Wakorintho 12).

Familia iliyokuwa karibu na jumuiya ya Wakristadelphiani, kwa mshangao katika karne ya kwanza baada ya Kristo, ni Wayahudi walioamini kwa sababu ndipo ulipo msingi wa jumuia yetu. (Mathayo 4:23, 6:2, 9:35, 10:17; Matendo ya Mitume 9:20, 13:5, 14-15, 18:4, 7-8, 26; Ufunuo. 2:9, 3:9). Na hii ndiyo sababu moja ni kwa nini Wakristadelphia wametambulikana kuwa ni aina ya Uyahudi wa Kimasihi; yaani wale walio na imani ya Wayahudi katika ahadi alizoahidiwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo wanaomwamini Bwana Yesu Kristo kuwa ndiye Masihi. Wakristadelfia wapo tofauti kabisa na makanisa ya Kikristo yanayowazunguka. Utaratibu huu huu sio wa kawaida kabisa, na wala watu walio wengi hawauelewi sana.

Ushirika ndiyo kiini cha njia ya maisha ya hawa Wayahudi. Ni ushirika ndiyo unaowaunganisha pamoja Wakristadelfia na wakafanyika kuwa mwili wa Kristo (Waefeso 4:12). Na ingawa hawa ndugu wanaishi maeneo tofauti na kufanya kazi tofauti lakini wote kwa pamoja kiini cha mwongozo wao ni Neno la Mungu (Zaburi 119:105), katika umoja mkamilifu (Warumi 12:4-5) ukijengwa juu ya msingi wa kanuni za Biblia ambazo zinaaminiwa na kukubaliwa kuwa ndiyo nguvu ya mwongozo wa maisha yetu (Yeremia 10:23) ili kutuongoza tupate wokovu (2Timotheo 3:15-17).

 

Na watu wengi hawazifahamu hasa njia za msingi wa maisha ya jamii hii jinsi wanavyoishi kwa upendo na umoja, na hasa katika mazingira ya Afrika. Mawazo mengi kwa ajili ya kufanyakazi pamoja kwa ajili ya wote ni jambo ambalo ni kinyume cha asili katika utamaduni wa Kanisa, wakati wa ukoloni na katika asili ya utamaduni wa Kiafrika .

Kozi hii imetayarishwa ili kuelezea kwa kina njia ya maisha ya Wakristadelfia.

 

Kozi hii imeandikwa kwa ajili ya nani?

Kwa huzuni na aibu, tunakiri kutambua ya kwamba katika miaka ya hivi karibuni (tunapoandika katika Mwaka 2019) na hasa katika Tanzania, ingawa hali hii ipo hata katika nchi zingine pia, mambo mengi ya karne hiyo ya kwanza ya maisha ya Kibiblia ya Wayahudi yamesahauliwa na kupotea. Tumeruhusu mawazo ya kibinadamu kuingilia kati mafundisho safi ya karne ya kwanza (Zaburi 12:6). Na matokeo yake kukosekana kwa umoja na kusambaratika kwa jumuia iliyopo Tanzania (2Wkorintho 6:15). Watu, wapotofu wamejichukulia nafasi ya iliyozoeleka ya uongozi wa makanisa ya asili kwa sababu ya kutoifahamu kweli, watu wasio fuata utaratibu, wasio na matumaini na kwa kajili ya uchoyo na ubinafsi.

 

Kosa kubwa ni kuwa ufahamu mdogo wa kuhusu ushirika. Kama tunajenga juu ya msingi dhaifu, basi nyumba yote itaanguka (Mathayo 7:26). Na matokeo yake ni uharibifu uletao maangamizi. Ndugu, ambao ni wanaume na wanawake 2,500 wameshabatizwa katika Tanzania; lakini baada ya kuwepo Eklesia 25 zenye waumini 100 (kama tulivyotazamia); na sasa hakuna kundi lililo na waumini 30, waumini wengi sasa wanaishi katika hali ya upweke kabisa, ambapo kila mmoja anajitahidi kuishi “maisha ndani ya Kristo” akiwa mtu mmoja pasipo kuwa na msaada wowote. Lakini, tunaagizwa na Bwana ya kwamba tunahitaji kukutanika pamoja ili tuweze kuingia katika ule Ufalme. Tunatakiwa tuache tabia ya kimwili na tulifahamu somo hili kwa ukamilifu.

Tukiufahamu ushirika(kukukusanyika pamoja) ni wa muhimu sana ikiwa tutaunganika pamoja katika Eklesia (Wafilipi 2). Tunahitaji kukusanyika pamoja katika imani na upendo, ili kama tutajikwaa tunapotembea katika njia ile nyembamba iendayo kwenye Ufalme ndipo sasa ndugu yetu yaani mwanaume na mwanamke atatushika sisi mkono na kutinua (Mathayo 7:14).

 

Basi,kozi hii ni kwa ajili ya mtu yeyote ambaye anahusika kwenye huduma yoyote katika Wakristadelfiani. Hata kama ni watoto wadogo katika Sunday school (shule ya jumapili), au wanaojifunza Neno ili wabatizwe, ama ndugu mwanamume au mwanamke, na hata kama ni mzee aliye ndani ya jumuiya ya waumini. Kwa sababu sisi sote tunahitaji kuelewa ushirika (kukusanyika pamoja). Na wote tunahitaji kuhusika kwenye umoja thabiti katika kukutanika pamoja(ushirika).

 

Je,utafaidikaje kwa kusoma kozi hii

Kila tunapoingia jambo lolote jipya maishani mwetu, tunaujiuliza swali, “nitapata faidika gani katika jambo hili? Na kama hilo ndilo swali unalojiuliza hivi sasa, basi ni dhahiri ya kuwa unakosa shabaha ya kufahamu nini hasa maana ya kuwa Mkristo. Watu wengi hujiunga na Makanisa ili wapate maslahi binafsi. Na wengine wanaingia makanisani ili wafaidike zaidi na zaidi. Jambo hili ni la kweli hasa katika Afrika ambako wapo “wazungu” wanaopenda kutoa ili wajionyeshe mbele za watu. Watu wengi huingia kanisani ili wapate ukarimu na wema kutoka kwa matajiri “wazungu” matajiri. Ni waatu wachache kabisa, kwa kweli, wanaoingia katika kanisa ili waweze kuwasaidia wengine. Na tuyakumbuke maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe:Ni heri kutoa kuliko kupokea” (Matendo ya Mitume 20:35).

.

Ni kanuni ya Biblia kwamba Ukristo siyo ni kiasi gani cha fedha tunachoweza kupata, na wala siyokujihakikishia kwamba tumo ndani ya Ufalme wa Mungu (ingawaje inatumainiwa kuwa hili ndilo litakuwa ni matokeo ya matendo yetu). Ukristo ni kuhusu kujengana ndani yetu, mmoja na mwenzake katika tabia za Mungu, ili tuweze kumpendeza Mungu mwenyezi (Hesabu 14:21; Yohana 17:21) ili kwamba tuwe mmoja katika yeye na pamoja na Mwanaye. Ukristo una maana ya kukusanyika pamoja!

Kozi hii itakufundisha jinsi ya kuwa Mkristo wa kweli.

Kusudi ya kozi ni nini ?

Kozi hii imegawanyika katika sehemu kuu nne:-

 • Jumuia ya Wakristadelfiani ni nini?

 • Kufanya kazi pamoja

 • Meza ya Bwana

 • Kazi zetu.


 

Vichwa vya habari vya sehemu hizi nne vinajieleza na kujifafanua vyenyewe. Ingawaje sehemu hizi hazitosherezi kila suala la somo la (ushirika)kukusanyika pamoja, ni matumaini kwamba wakati utakapokuwa umeyasoma masomo yote ishirini utakuwa na umefahamu na kuwa na maarifa mengi kuhusu mambo yale yanayotakiwa katika maisha ya kweli ndani ya Kristo. Maeneo yaliyozungumziwa katika masomo yote sitini, kama vile kuchagua kazi zetu, uchoyo, hasira na uvumilivu tutaweza kuyaelewa zaidi.


 

Jinsi ya kutumia kozi hii

Ni jambo la kawaida kusoma “ni makala nzuri” katika kipeperushi,na kisha tunakiweka chini na kufikiria, ““Hmmm, ilikuwa makala nzuri, ninakubaliana na yote makala(kifungu). Na kisha tunaweka kipeperushi chini na tunasahau moja kwa moja kile ujumbe uliosemwa.Na wala hakuna tofauti kabisa na jinsi tunayoishi (Kutoka 24:7; Kumbukumbu la Torati 17:19; Mathayo 21:42).

Nyakati zingine, tunachukua ((kifungu)makala na tunasema, “Ndugu x anahitaji kusoma kifungu hicho”. Na Ndugu x anahitaji kuyabadili maisha yake kutokanan na yale yanasemwa na kifungu kile” - na kwa hiyo mara kwa mara hatuoni kuwa ni sisi wenyewe tunaotakiwa kubadilika (Luka 6:41-42).

Tunaposoma maneno ya kozi hii,tunahitaji kuyalinganisha na kile kinachosemwa na Maandiko (Matendo 17:11). Kama kile kinachosemwa hapa kinapatana na Maandiko (ambayo tuna amini kuwa ndivyo yalivyo), basi na tusisahau, na tena ni lazima tutende kama yasemavyo Maandiko. Ukristo wa kweli unahusu kubadilika katika katika maisha yetu. Unahusu ushirika na Mungu.

 

Swali lililo kubwa ni “Kanisa ni nini?”

Jamii (jumuia)ya Wakristadelfiani kwa kawaida wanatumia toleo la Kiingereza lenye neno la Kiyunani : ekklesia (Ecclesia), wanavyojitambulisha wenyewe , na siyo neno kanisa.Neno hili lina maana ya asili ya “mkutano, usharika, baraza” kwa maana halisi kwa “kuhitimisha” maana ya neno ekklesia.

 

Ekklesia ni kusanyiko la waamini ambao wanashirikiana na Mungu. Hapa hatuzungumzii majengo, tunazungumzia kuhusu watu ambao ni waumini – “Maana tumejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni” (Waefeso 2:20).

Jengo, ndiyo, lakini ni jengo ambalo linaundwa na wanaume na wanawake, katika ushirika, unaoongozwa na Kristo Mwenyewe.

 


 

Swahili Title
Somo 1: Utangulizi – Kanisa ni nini?
Swahili Word file
Literature type
Sub type
English only