The End of the World

Swahili


Kadri jua linavyoanza kuchomoza, ndivyo Kweli inavyotiisha wazi wazi, hakuna kilichobakia. Maana hakuna mtu yeyote aliyeweza kuonekana; kila kiumbe chenye uhai kilikuwa kimeharibika, kilikuwa kimetoweshwa katika sura ya nchi.
Mabaki
Na bado, jambo la kushangaza, walikuwepo watu wachache ambao ni mabaki, ya familia moja waliokuwa wamefungiwa ndani ya nyumba yao- ilitengenezwa kuwa makazi, walimoweka mahitaji yao ambayo yange watosheleza kwa zaidi ya mwaka mmoja. Walikuwa wamesikia maonyo na walikuwa wamejiandaa, kwa kuwa muda ulipofika, waliingia na wanyama na vifaa vyote muhimu walivyoviona kuwa vitawafaa kwa ajilio yao na wanayama.
Mawazo yao yalikuwa bado yamezoea fikira za mambo yale waliyokuwa wameyaona kwa muda mrefu. Kwa kuanzia na tukio la wao kuwa ndani ya safina lilikuwa tukio la kutisha ; sauti ya nje ilikuwa yenye kuwatia hofu kubwa na ya  kuwavunja mioyo, na iliyosababisha mabadiliko ya makubwa ya kutisha na vurugu, lakaini familia ilikuwa imetulia pamoja na ahadi yao ilikuwa imetimizwa , walikuwa salama wakiwa wamefungiwa ndani. Na baadaye kulikuwa na ukimya ambao ulikuwa ni wakati mbaya sana. Na ilikuwa sasa hali ya namna gani? Je, ilikuwa salama kufungua dirisha? Je, wangeona nini?
Walifahamu hakika kuwa huko nje nchi ingekuwa katika tofauti na ya kutisha na mwonekano wake ungekuwa tofauti na sura yake ya mwanzo ya ulimwengu ambao waliokuwa wameuzoea walikuwa wameuacha nyuma. Makazi yao yalikuwa hayaonekani tena na alama ya mipaka (kama vile milima, mabonde nk ) ilitoweka  kabisa . Kulikuwa na utupu kabisa na uharibifu wa kutisha.
Je, wangekuwepo wa kuokoka?
Je,ni Ubunifu wa Sayansi?
Yamkini, unafikiria, kuwa huu ni ubunifu wa sayansi. Ni bahati ambazo huwa hazitokei tena. Ni ukweli usiopingika kuwa tukio hili liliwatokea watu kabisa. Ni ukweli wa habari ya familia moja iliyookoka wakati ulimwengu wao ulipoangamia.
 Hawakufahamu lolote kuhusu vita ya nyuklia au miozi; hatari iliyokuwa imewazingira wao yalikuwa ni mabilioni ya tani ya maji yaliyowazunguka kila mahali- mawimbi mengi makubwa na mbubujiko wa maji mengi sana yaliyoifuka dunia.  Hata hivyo, matukio haya ni muhimu kwetu, kwa kuwa hata sisi tunakabiriwa na maafa  makubwa ya ulimwegu, maa-ngazi makuu ya kutisha (hasa ya watu kwa kuchomwa moto, kuuawa kwa kutumia siraha za kivita, mabomu nk) badala ya  watu kuangamia kwa gharika ya maji na  pia kuna hofu kubwa  ya ulimwengu kufikia mwisho wake kama hofu waliyokuwa nayo wao  
Siku za Nuhu- Ni kama zilivyo siku zetu!
Unaweza kuisoma habari kamili ya Nuhu na gharika katika Biblia- katika kitabu cha Mwanzo (Mwanzo 6-8). Ingawaje Nuhu na familia yake waliishi miaka 5,000 iliyopita, sehemu ya ulimwengu wao haujatofautiana sana na huu ulimwengu wetu. Vitabu vya historia vinaeleza kuwa ukiangalia nyuma katika nyakati hizo watu wa zamani za kale walioishi zama za mawe hawakuwa wastaarabu, je, hauamini! Biblia kwa kweli inatuambia kuwa walikuwa wastaarabu walioishi katika miji au majiji, wakifanya starehe, wakipata utajiri, wali kula na kunywa vizuri, walikuwa na uhuru wa kufanya kama walivyopenda, hawakuwa na maadili. Kulikuwa na vitendo ya vurugu, uharifu, ukatili, watu wadhalimu na watesaji na ilikuwa sawa sawa na mambo yanayotenda siku hizi, maana hakika dunia imekuwa ni sehemu ya hatari kabisa.
Nuhu na pamoja na familia yake waliteseka na kuhuzunishwa na mateso waliyoyaona; waliutamani ulimwengu ulio bora ulio mzuri na wenye amani. Tofauti kubwa iliyopo kati yao na watu wengine walioishi wakati ule ni kwamba wao walimwamini Mungu Muumbaji na walifahamu kuwa anaitunza dunia na ndiye anaye wapatia wanadamu mahitaji yao.
Mungu akamwambia Nuhu na kusema   kuwa alihuzunishwa na kukasirika kwa sababu dunia yake ilikuwa imeharibiwa na alikusudia kuisafisha. Mungu akasema kwa uhalisia kuwa atamfuatilia mbali mwanadamu ambaye ameijaza dunia kwa uovu.
Mungu alimpatia Nuhu maelekezo jinsi ambavyo yeye na familia yake wangeweza kuwa salama  na wakati Nuhu , na mkewe,  na wanawe na wake za wanawe walipoingia ndani ya safina waliyoitengeneza, ni Mungu mwenyewe aliyefunga mlango wa safina. Familia iliishi ndani ya safina  yapata kama mwaka mzima mpaka maji ya gharika yalipo kauka na Mungu aliyekuwa  amewaokoa katika  ule msiba na maafa yale, aliwatia moyo  kwa kuwaambia watoke nje ili wakaanze maisha mapya.
Ahadi ya Upinde wa mvua.
Hakika ulimwengu wa zamani  ulifikia mwisho; haikuwepo dalili ya ustaarabu  tena au  kitu chochote ambacho kilikuwa kimetengezwa kwa uwezo wa mwanadamu hakikuwepo, lakini sasa dunia ilikuwa ni salama  na ikawa tayari kukaliwa na watu na dunia ilimsubiri Nuhu apande mbegu impatie mavuno mengi. Mungu alikuwa bado na kusudi na sayari hii ya dunia. Kwa kweli Mungu mara moja akampatia Nuhu ahadi muhimu sana.
 “Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya. 22 Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma”.  (Mwanzo 8:21,22).
Kama dhamana Mungu aliweka ishara - upinde wa mvua ambao huwa unaonekana angani wakati wa mvua (Mwanzo 9:14-16).
Ahadi hii alipewa ingawa Mungu alifahamu kuwa uzao wa Nuhu( ambaye  katika yeye  wametokea asili ya wanadamu wote  na mataifa yote ya dunia) wasingekuwa wazuri kuliko  watu walioishi kabla ya gharika, kwa sababu kwa kunukuu tena maneno ya Mungu: “maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote”. Hii ina maana kwamba kila mmoja wetu amerithi hali ya kutenda dhambi kutoka kwa wazazi wa kwanza( Adamu na Hawa)  uchoyo ambacho ndicho kiini kinachorahisisha kuleta chuki badala ya kupenda na uchoyo husababisha uharibifu na kifo. Kama tukiachiwa pekee yetu hatuna uwezo wa kubadilisha asili hii ya kutenda dhambi na wala hatutakuwa na tumaini la kutunza ulimwengu.
Mungu alimthibitishia Nuhu alimwokoa lakini hatimaye Nuhu na familia yake walifariki.
Bado kuna mateso na kifo duniani kwa hiyo kulikuwa na sababu gani ya wao kuokolewa? Ilikuwa ni raha gani ya Nuhu kuahidiwa kuwa dunia ingeendelea kuwepo kama alikuwa haendelei kuishi ili kuifurahia?
Ni muhimu tusome Agano Jipya ambapo tutagundua jambo lililomsukuma Nuhu. Ndipo tunapoambiwa Nuhu alimwamini Mungu kuwa atampatia thawabu wakati ujao hata inagwa alikufa, na “atakuwa mrithi wa haki” (Waebrania 11:7). Nuhu akafa katika Imani alifahamu kuwa ataishi tena katika dunia wakati itakapo safishwa yote, wakati ambapo yeye na watu wengine wenye haki kama yeye watakaokuwa hawana dhambi, watu wasiokufa tena, lakini watakuwa wamebadilishwa na kuwa wenye haki, waishio milele; wakati mambo ya dunia yaliyotengenezwa na wanadamu yatakapotoweka na mambo ya Mungu aliyoumba kwa ajili ya dunia yatakapoanza
Ulimwengu Mpya
Ingawa baada ya gharika nchi iliendelea kuwa na tamaa kama vile ilivyo kuwa mwanzo, naye Mungu alikuwa amesha anza kuubuni ulimwengu wake. Hakukusudia tena dunia kujawa na mateso na kifo milele. Haya ni baadhi ya makusudi ya Mungu kwa maneno yake katika Biblia:
" Maana Bwana, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine. . . Wala hapana Mungu zaidi ya mimi; Mungu mwenye haki, mwokozi; hapana mwingine zaidi ya mimi.
Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine.
 Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine.  Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa. Nao watasema, Kwa Bwana, peke yake, iko haki na nguvu “(Isaya 45:18-24).

“Kwa maana dunia itajazwa maarifa ya utukufu wa Bwana, kama maji yaifunikavyo bahari " (Habakuki 2:14).
Mungu mwanzo alimfunulia mpango wake mtu aliyeitwa Ibrahimu, ambaye alizaliwa Mashariki ya Mbali yapata miaka 1000 baada ya Nuhu. Ibrahimu alimwamini na akaambiwa kuwa katika uzao wake mataifa yote watabarikiwa.  Kama vile Nuhu, Ibrahimu pia alifahamu ile ahadi ya kuwa ni uzima wa milele utakaokuwepo baadaye wakati ulimwengu wa Mungu utakapokuja katika dunia, alifatambua kwamba atakuwa “: mrithi wa ulimwengu” (Warumi 4:13).
Ibrahimu- Mzazi wa Yesu Kristo
Mungu alimwahidi kumpatia Ibrahimu na uzao wake nchi, na katika Ibrahimu ilitokea nchi ya watu, Wayahudi. Wakati Wayahudi walipoishi katika nchi ya Israeli walifanyika kuwa Ufalme - kwa hakika ulikuwa Ufalme wa Mungu duniani- ili uwe mfano wa haki na amani kwa mataifa yote. Mji wao mkuu, aliouchangulia na Mungu, ulikuwa Yerusalemu, mahali hekalu, Nyumba ya Mungu, iliyojengwa kwa heshima na utukufu wake.
Lakini Wayahudi kama taifa hawakuweza kuuokoa ulimwengu, ingawa walionyeshwa ishara na maajabu na walipewa msaada na maagizo kutoka kwa Mungu. Baadhi ya Wayahudi waliamini na kutii lakini wengi wao walipenda kuenenda katika njia zao za uovu.
Tabia ya kidunia ya Wayahudi iliwazuia wasiweze kuwa Ufalme wa Mungu  hadi Mungu alipomtuma Mwana wake, Yesu Kristo, ambaye ni Myahudi kwa kuzaliwa  wa ukoo wa Ibrahimu , na alizaliwa na Mariamu, ili kuokoa watu wa Mungu kutoka katika dhambi na kifo ili atawale Ufalme.
Kuzaliwa kwa Yesu ulikuwa ni mwujiza na hata maisha yake yalikuwa ya kipekee kabisa. Aliwaonyesha watu jinsi iwapasavyo kuishi, aliwaonyesha watu jinsi wanavyotakiwa kujifunza jinsi ya kuwajali watu wengine badala ya kujipenda wao wenyewe na badala ya kuweka chuki katika mioyo yao waweke upendo .Yesu aliweka dhahiri kuwa ulimwengu wa Wayahudi ungefikia mwisho.  Viongozi wa Wayahudi walikuwa wanafiki, ambao kwa nje walijifanya wacha Mungu na wenye haki lakini kwa ndani walijaa uovu. Hekalu lilikuwa ni “ pango la wanyang’anyi” badala ya kuwa “nyumba ya sala” (Mathayo 21:13) na ingeharibiwa , pamoja na mji wa Yerusalemu, nao Wayahudi wangetiwa utumwani na kutawanywa duniani kote.
"Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani"
Kwa wale wamwaminio na kumfuata, Yesu aliwapatia ujumbe wa matumaini na habari njema kuhusu Ufalme wa Mungu. Aliwaambia waombe Ufalme uje nayo mapenzi ya Mungu yafanyike “hapa duniani kama mbinguni" (Mathayo 6:10). Yesu aliwahakikishia wafuasi wake  kwamba kwa maana jinsi hii Mungu uliupenda ulimwengu  hata akamtoa Mwanawe  pekee kuwa Mwokozi, ili "kila  mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima  wa milele " (Yohana 3:16);  na kuwa yeye ndiye " ufufuo na uzima" na atawafufua wafu (Yohana 5:25-29).
Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba atakuja " juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi" (Mathayo 24:30); na kiti chake cha enzi kitakuwa Yerusalemu; atayatawala mataifa yote na wanafunzi wake waaminifu wataurithi Ufalme, watatawala pamoja naye dunia yote (Mathayo 25:31-34).
Viongozi wa Wayahudi walikataa kumwamini Yesu Kristo kuwa ni Mwana Mungu, Mokozi wao na Mfalme na wafanya njama ili kumwua. Kwa hiyo alisulubiwa na kufa (Mathayo 27). Hii ilikuwa ndiyo gharama aliyolipa Mumgu ili kuuokoa ulimwengu! Mwanawe pekee, mpendwa wake, ambaye aliwaonyesha watu jinsi Mungu alivyo, Mwokozi, ambaye alizaliwa ili awe Mfalme, aliuawa na watu waovu
Uadui kati ya wafuatao Roho na wale wnaoifuata Dunia
Mpango wa Mungu ulifikia hali ya hatari. Hapa kuna kuna uadui kati ya wale wanaofuata roho na wale wanaofuata (ulimwengu) dunia, wakikabiliana uso kwa uso. Upande mmoja ni wale wanaomfuata Mungu, ambao unawakirishwa na Mwanawe , Mfalme mwenye haki aliyeonyesha  anayefahamu Kweli ya Mungu na msamaha wa dhambi na mwenye kujali na mwema- hata hivyo, ingawa hakuwa na kosa, kila wakati alikabiliwa na nguvu ya upinzani wa watu waovu. Na kwa upande  mwingine,  ni watu wale wanaofuata (dunia)ulimwengu wenye kuchochewa na chuki, ambao nguvu zao  ni unyanyasaji, uchoyo, dhuruma na uharibifu.
Katika Yesu Kristo, Mungu alileta suruhisho la laana ya dhambi na kifo. Alionyesha kuwa kifo siyo tatizo kwa Mungu. Kwa kuwa a angeweza kumfufua mtu aliyekufa. Mwanawe ambaye kamwe hakutenda dhambi alifufuka kutoka katika wafu siku ya tatu baada ya kufa msalabani, na sasa anaishi milele. Aliwatokea wafuasi wake na akazigeuza huzuni zao kuwa mshangao kwa shangwe na akageuza uchungu wao kuwa furaha (Yohana 20; Luka 24:36-48). Yesu aliwaambia bado wakati haujafika wa kuusimamisha Ufalme wa Mungu hapa duniani. Alipaswa aende mbinguni kwa Baba yake, lakini amepewa mamlaka yote ya mbinguni na duniani. Wanafunzi wake walitakiwa kwenda duniani kote, waihubiri Injili (Habari njema za Mungu), na kufundisha watu amri zake na kuwabatiza kwa jina la Yesu Kristo ili kupata ondoleo la dhambi. Na Yesu aliwa ahidi: “Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari" (Mathayo 28:18-20).
Wanafunzi wa Yesu walifahamu kuwa “ukamilifu wa dahari” utafika wakati Yesu atakaporudi na kuusimamisha Ufalme wa Mungu, na wakati huo atawafufua waliokufa ambao walikuwa waaminifu kwa Baba yake na kwake  yeye , nao watapewa uzima wa milele  na watatawala pamoja naye  hapa duniani.
Wakati Yesu aliposema kuwa atarudi, alifafanua wazi wazi kuwa ulimwengu-utakuwa  katika wakati wa dhiki kubwa na hasa alisema kuwa itakuwa kama  vile zilivyokuwa siku za Nuhu. Akawaambia kuwa:
"  Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu." (Mathayo 24:38,39).

Kama vile zilivyokuwa Siku za Nuhu!
Kutoka mbinguni Yesu alituma ujumbe kwa mitume wake. Alisema ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, Iko wapi ile ahadi ya kuja kwa ufalme? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.
 Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu;
 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.
 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.
 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.
 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
(2 Petro 3:3-10; pia soma Matendo ya Mitume 17:31  na 2 Wathesalonike 1:6-10).

Je, yatakuwa Maangamizi ya Nyuklia?
Kwa hiyo, wakati Yesu atakaporudi kuusimamisha Ufalme wa Mungu, je, dunia yetu itaangamizwa kwa moto? Wakati Petro na Paulo walipoandika maneno hayo uwezekano wa  wanadamu kuwa na uwezo wa kuangamiza dunia kwa moto ni mawazo yaliyokuwa  juu ya uwezo wao wa kufikiri. Laakini katika siku zetu hizi hakika ni jambo la kweli linaloogopwa sana. Hakuna siri tena kwa kuwa kuna siraha za kutosha za Nyuklia za kuweza kuteketeza kila kiumbe chenye uhai katika uso wa dunia na kuiacha ikiwa haina kiumbe hai na ikiwa imeharibiwa.
Je, hili limetabiriwa katika Biblia? Je, itakuwepo vita ya Nyuklia?
Tuaangalie uthibitisho mwingine katika Biblia, tukumbuke kuwa Yesu aliyathibitisha yote yaliyotangulia kunenwa na manabii katika Agano la Kale, ambaye alitabiri kwamba makao makuu ya matukio yote yatakuwa Yerusalemu, katika nchi ya Isreali.
Unabii mwingi ulitabiriwa mamia ya miaka iliyopita na sasa tunashangaa  mambo yaliyotabiriwa yanapotia wakati huu ulimwenguni. Unabii unazungumzia kuhusu Israeli  na wana wa Israeli kuwa ndiyo ushahidi mkubwa kuhusu Mungu katika mataifa yote, na Yerusalemu kuwa kiini cha matatizo na mataifa kama Umedi(Irani), Libya, Ethiopia na taifa la kaskazini kubwa lenye nguvu , lenye zana za siraha za maangamizi, zimeanza kuwa tishio la amani ulimwenguni na hizi nchi zimekuwa zikiishambulia Israeli.

Unabii  mwingi ulitimia Kweli
Kwa mfano nabii Ezekieli (sura za 38-39) zinatabiri kuhusu uvamizi wa kutisha dhidi ya taifa la Israeli katika “ miaka ijayo” baada ya watu wa Israeli kutoka katika nchi walizokimbilia na kurudi  tena katika nchi yao. Jeshi kubwa mno kutoka wataivamia Israeli, lakini Mungu ataingilia kati ili kuiokoa Israeli:
" Hakika katika siku ile kutakuwako tetemeko kubwa katika nchi ya Israeli;  hata samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama wa kondeni, na vitu vyote vitambaavyo juu ya nchi, na wanadamu wote walio juu ya uso wa nchi, watatetemeka mbele ya uso wangu; nayo milima itatupwa chini, na magenge yataanguka, na kila ukuta utaanguka chini.
Nami nitaita upanga, uje juu yake katika milima yangu yote, asema Bwana MUNGU; nao upanga wa kila mtu utakuwa juu ya ndugu yake “(38:19-21).
Mungu atawanyeshea mvua  nyingi mno, na kuwatupia mawe makubwa  na moto  nao wataanguka juu ya  milima ya Israeli.  Nayo Vita itawafikia hata watu walio mbali wakaao salama (39:6).
Israeli makao makuu ya mataifa yote
Na kisha, tuna ambiwa kuwa ,hao waishio katika miji ya Israeli watatoka ili kukusanya siraha, ambazo zitatumika kwa ajili ya kuni kwa muda wa miaka saba (39:9,10). Na pia watakuwepo makundi maalum kwa ajili ya kuzika, watakuwa na ujuzi wa kuzika watu waliokufa; na kila mfupa utakusanywa (kuokotwa) na utazikwa kwa uangalifu sana. Maelezo ya kina kuhusu tukio hili yanatisha sana kwetu sisi katika kipindi hiki chenye siraha za nyuklia, tunafahamu uwezo wa siraha za nyuklia na madhara yatokanayo mionzi ya sumu ya nyuklia.

Nabii Yoeli pia alitabiri kuhusu Siku ya BWANA:
“Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi.  Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo." (2:30,31).
Kwa kinywa cha Malaki, nabii wa mwisho katika Agano la Kale, Mungu alisema:
"Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi." (4:1).
Lakini ingawa ni wanadamu wanaopigana vita hivi, Mungu anawatumia ili kutumiza kusudi lake.
"Tazama, siku moja ya Bwana inakuja, ambayo mateka yatagawanyika kati yako.
 Kwa maana nitawakusanya mataifa yote walete vita juu ya Yerusalemu; na huo mji utapigwa, nazo nyumba zitatekwa, nao wanawake watatendwa jeuri; na nusu ya watu wa mji watatoka kwenda utumwani; ila mabaki ya watu wa mji hawatakatiliwa mbali.
Hapo ndipo atakapotokea Bwana, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita.
Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini. " (Zechariah 14:1-4).
Mataifa yenye nguvu za kijeshi tayari ya meshajiandaa kwa ajili ya vita ya Mashariki ya mbali.Na siyo vigumu kuwaza kuyafikiria mataifa hayo yanavyokusanyika pamoja kwa ajili ya vita ya mwisho katika nchi ya Israeli. Taifa dogo litakuwa ndiyo kiini cha vurugu kwa ajili Vita ya Tatu ya Dunia.
Na hakuna shaka kuwa unabii wote unaohusu vita hii utatimia mapema miaka ya karibu. Lakini , na sisi kama Nuhu, tunaweza kuwa na ujasiri katika Mungu ikiwa tunatii maagizo ambayo ametupatia katika Biblia, tukifahamu kuwa ataruhusu  machafuko na ghasia  na atailinda dunia sawasawa na ahadi yake.
Je, ni kweli dunia itateketezwa kwa moto? Na, je, sayari hii nzuri itaangamizwa?
Siyo dunia itakayoangamizwa, lakini ni huu ustaarabu, wanadamu waipendao dunia (anasa) kuliko kumpenda Mungu ndiyo watakao angamizwa.
Itakuwaje kuhusu Huzuni na Kifo?
Kwa kuwa huzuni na kifo havitakuwepo milele. Mambo yote yaliyone katika unabii wa nyakati zote utakamilika kwa kuthibitisha furaha na tumaini
“Nami nitajitukuza, na kujitakasa, na kujidhihirisha, mbele ya macho ya mataifa mengi; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.” (Ezekieli 38:23).
Yoeli anasema:
" Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama BWANA, alivyosema. " (2:32).
Malaki anathibitisha kwa faraja ya maneno ya Mungu:
“Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa mazizini.” (4:2).
Kwa maana Zekaria huthibitishia kuwa,
“Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja. " (14:9).
Ni mwisho wa Falme za Ulimwengu
Ulimwengu hautamkaribisha Yesu kuwa Mfalme.  Watu wengi waliopata utajiri na wakuu wenye vyeo watampinga lakini tunaambiwa kuwa falme na mamlaka zao zitaharibiwa kabisa, zitateketezwa kwa moto, nao watazidharau kazi zao wao wenyewe! Nao walio pata hasara ya utajiri wao wataomboleza, wakati miradi mikubwa, migodi ya madini na visima vya mafuta, zana za vita na siraha za kemikali, mamlaka ya ukuu wao, vyombo vya anasa, vyombo vyao vya usafiri, mifumo ya taasisi zao za fedha (mabenki)- vyote vitateketea kwa moto! (Soma Ufunuo 17; 18; 19).
Biblia ni kitabu cha Mungu chenye mwongozo wa maisha. Kinaelezea ushauri dhahiri – na pia kina maonyo ya kutisha. Watu wale wanaofuata ushauri wa Mungu, kama vile Nuhu alivyofanya, wataokolewa katika hukumu ile ya kutisha ambayo Mungu ataileta duniani.
Wale watakaoamini na kufurahi kwa kumkubali Yesu, pamoja na waaminifu wote wanaume na wanawake wa nyakati zote , na wale watakaofufuliwa kutoka katika wafu, watasema:
“Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele. Na wale wazee ishirini na wanne waketio mbele za Mungu katika viti vya enzi vyao wakaanguka kifulifuli, wakamsujudia Mungu
 wakisema, Tunakushukuru wewe, Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa sababu umeutwaa uweza wako ulio mkuu, na kumiliki.
Na mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, na hao walichao jina lako, wadogo kwa wakubwa, na wa kuwaharibu hao waiharibuo nchi." (Ufunuo 11:15-18).
Mwanzo Mpya
Kwa hiyo mwisho kwa kweli ndiyo huwa ni mwanzo . . .  ni mwanzo mpya ambao sisi wote tutaweza kushiriki
Kwa kuwa jua linapochomoza huangaza hata kitu chochote kisiweze kujificha… Kila kitu kitakuwa kimefanywa kipya! Nayo dunia itazukiwa na nuru ya utukufu, nazo kelele za shangwe zitapaa mbinguni (Isaya 65:17-25; Ufunuo 21:1-5).
“Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.” (Ufunuo 21:4).
-- SHEILA WILSON

 

Swahili Title
Mwisho wa Ulimwengu
Literature type
English only
D7 Node Id
951